Karibuni wote kwenye tovuti ya Kanisa la Biblia Publishers
Hongera kwa nia yako ya kusoma Neno la Mungu. Tunategemea tunaweza kukusaidia kwa njia mbalimbali ili ulielewe na kulitangaza Neno la Bwana na kueleza ujumbe wa Yesu Kristo kwa watu walio karibu na walio mbali. Chunguza tovuti hii vizuri ili ujipatie vitabu vinavyofaa kwa maisha na huduma yako. Vitabu vyetu vinapatikana katika maduka mbalimbali ya Kikristo katika nchi ya Tanzania.
MPYA
Ufafanuzi Hai wa Biblia (Believer‘s Bible Commentary) unaeleza Waebrania, Nyaraka Saba za Kanisa na Ufunuo wa Yesu Kristo. Mafungu magumu yanafafanuliwa kwa maneno rahisi na kwa lengo kumwandaa Mwamini kwa siku za mwisho, pamoja na nyongeza za majedwali na ramani.


EMMAUS SCHULE YA BIBLIA KWA YA POSTA
inahudumia watu wote wanaopenda kusoma Biblia kwa njia ya posta. Masomo na mitihani yanatumwa kwa mwanafunzi. Baada ya kujaza anarudisha mtihani na malipo kwenye ofisi zetu.
​
Tuma maulizo kwa SMS, Simu au whatsapp +255 765 442 452
Email: emmaus.dodoma@kanisa-la-biblia.org
Inawezekana kusoma Emmaus kwa njia ya mtandao. Pakua Emmaus-App kwenye simu kwa kutumia playstore. Kusoma kwenye mtandao ni bure.
Jina la Emmaus linatokana na jina la kijiji kimoja katika Biblia ambako wanafunzi wawili walikuwa wanaelekea walipotokewa na Bwana Yesu baada ya kufufuka kwake, na alipokuwa anawaelezea maandiko, Luka 24:13.
UKITAKA KUPATA MAELEZO ZAIDI
Hapa unaweza kuagiza orodha yetu ya bei za vitabu.